Muziki wa Christina Shusho anavyofunza upendo wa kweli

Na Beda Msimbe JARIDA la Mtandaoani la Golden woman limeandika makala ya kumweleza msanii wa muziki wa injili nchini Christina Shusho kam...

Na Beda Msimbe JARIDA la Mtandaoani la Golden woman limeandika makala ya kumweleza msanii wa muziki wa injili nchini Christina Shusho kama moja ya wanamuziki wachache wa Injili wanaofanya vyema kimuziki hapa nchini na duniani kote ambako muziki wa injili wa lugha ya kiswahili unasikika. Pia jarida hilo limeelezea maana ya nyimbo za mwanadada huyo katika maisha ya binadamu mintarafu kuabudu, kuomba na kusifu. Shusho akiwa katika miaka yake ya arobaini ameelezwa na mwandishi wa makala hayo katika lugha ya kiingereza, kuwa ni msanii ambaye amekuwa na wafuasi wengi zaidi mtandaoni wanaofuatilia muziki wake katikiakipindi cha miaka 20 sasa. Charles Mwangi alinukuliwa na https://goldenwoman.org/ kwamba unapomtafuta msanii wa muziki wa injili katika lugha ya kiswahili kwa namba ya vibao alivyotoa, idadiya watu wanaotembelea kupiga muziki wake na anayeongoza katika grafu, Christina Shusho anaongoza mpaka sasa. Anasema kwa dunia yenye wazungumzaji wa kiswahili milioni 150, Christina Shusho kwa takwimu anaonesha kutamba miongoni mwa wanamuziki wa Injili wa kike. Akiwa katika miaka yake ya arobaini, Shusho amekuwa na sauti ile ile aliyoanzia safari miaka 20 iliyopita, huku akiendelea kutoa vibao vikali zaidi ya kumsifu Mungu, kumtukuza na kuomba hisani yaani muziki wa maombi. Ukipanga idai ya muziki ambao ameshautoa mpaka sasa ukatafuta wastani unabaini kwamba kila mwezi mwanadada huyo amekuwa akitoa kibao kimoja cha kuzungumza na Mungu ama katika maombi au katika kusaka hisani. Binti huyo aliyezaliwa Kigoma, kwa kuendelea kung'ang'ania katika muziki huo ameonesha umahiri katika huduma yake kwa kutokuwa mchoyo wa nyimbo kwa kuendelea kuzitengeneza huku wakati mwingine akishirikiana na waimbaji vinara na hata chipukizi. Kwa kizazi cha miaka ya 2000 watakuwa wanamwelewa vyema kwa nyimbo zake kama “Wa Kuabudiwa” iliyomo katika albamu ya 'Unikumbuke.” Kiukweli wasanii wengi wa muziki wa injili huja na kuondoka,lakini mwanadada huyu ambaye mkononi ana albamu nane zenye jumla ya nyimbo 80, amekuwa tofauti kwani mwaka hadi mwaka amekuwa akikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa injili huku kila albamu yake ikiwa na ujumbe mahsusi kwa wanadamu unamhusu Mungu. Akiwa na historia ya kuanza kuimba tangu katika shule ya mafunzo ya dini ya watoto wadogo (Sunday School) mkoanio Kigoma, alipofika kuanzamaisha Dar es Salaam aliingia katika kwaya ya kabla ya kuanza kurekodi solo muziki wa injili; na kutoka wakati huo hajarudi Snyuma akichangia kwa kiasi kikubwa uamsho wa mapenzi kwa Mungu kupitia nyimbo zake. Sauti yake ya kuvutia na kupendeza, inayokua ikiwa katika nakshi ya mambo ya kawaida yanayofuata mistari ya Kibiblia imeondokea kupendwa na watu wengi na kumpeleka kimataifa. Mwaka huu akiwa anadaa albamu ya shusha nyavu tayari vibao vyake ikiwamo ya shusha nyavu vimekuwavitamba mtandaoni vikionesha kwamba vitakimbiza kuliko "Kitu Gani Kinitenge Na Upendo wa Bwana," na "Nipe Macho Nione". Ukifanya tathmini ya muziki wake unaona kwamba unasambaa kwa kasi kama moto katika vichaka kutoka nyumbani Tanzania, Afrika Mashariki na duniani. Katika kuonesha kwamba anakubalika mdada huyu ameshafanya ziara za maonesho katika nchi za Marekani, Uingereza, Austria, Canada na kadha wa kadha Huku Kenya ikiwa kama nyumbani kwake. Katika utafiti uliofanywa na mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha SAUT kilichopo Mwanza binti huyu aliyefungua chaneli ya You Tube Machi 15,2013 ilipofika Septemba 2021 alikuwa na watu waliotembelea chaneli hiyo milioni 43 ambapo ukitafsiri ni kwamba kila siku muziki wake umekuwa ukitembelewa na watu 15,000 katika kipindi cha miaka minane na hii si idadi ndogo hata kidogo. Ukiamngalia zaidi unaona kwamba ukijumlisha milioni 43 kwenye chaneli yake naidadi ya watu waliotembelea saiti nyingine mbalimbali wapatao milioni 40 unaona kwamba hakika Shusho yupo juu katika muziki wa injili wa kiswahili. Utafiti wa mwanafunzi huyo unaonesha kwamba kwa vijana wanaouzamuziki kidijiti huwahawakosi mnyimbo za mwanamuziki huyo na kumfanya kuwa mwanamuziki pendwa wa injili kwa sasa. Ukipanga albamu za Christina Shusho toka anaanza kuimba kwa mpangilio huwezi kupata hadithi nzuri ya Biblia au hadithi inayomhusu Christina Shusho, lakini ukichukua albamu zote ukasikiliza kwa mpangilio wa mahitaji utagundua kwamba kuna mambo muhimu ambayo Shusho anataka kukueleza kuhusu safari nzima ya maisha hapa duniani . Katika albamu hizo nane bila mpangilio wa siku zilipotoka bali kuzingatia mtiririko unaona amefanyakazi ya ziada kuzungumzia wokovu na safari yake pia kuhusu mwenendo wa walimwengu katika vita vya utu dhidi ya karaha zilizopo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwa mwisho mwema. Hadithi yake kisanii ipo " Nipe Macho Nione"; "Nataka Nimjue"; "Ongoza Hatua Zangu";"Wataka akutendee nini":" Unikumbuke"; "Shusha Nyavu" na" Relax". Katika dunia yetu hii iliyojaa vurugu kuanzia katika maisha ya kimwili hadi ya kiroho tangu wazazi wetu wa kwanza kuvurugana na Mungu kwa kuonesha kiburi cha kutojali maagizo waliyopewa, haja ya kuwa na macho ya kuuona ukweli ni lazima iwepo , macho ya katika roho si macho tu yanayotuwezesha kuona na kutafakari mambo ya kidunia. Ndio kusema Shusho amefanya vyema katika kutunga simulizi la maisha ya biandamu kupitiamistari yaBiblia na nyimbo zake zinazokupa maono ya uwezo wa wewe kuamua kati ya mambo mengi unayotakiwa kuyaamua ikiwamo ufuatiliaji wa maagizo mbalimbali ambayo Mungu aliyatoa moja kwa moja kwa watu watumishi wake waaminifu kama Musa, Adam na hata Abraham. Biblia imejipambanua kama kitabu ambacho kina maelekezo na wakati mwingine ya kimigongano, lakini kama huyo unayetaka kumwabudu anataka umwabudu katika roho na kweli unalazimika kuomba macho, macho yenye upekee wa kumuona Mungu katika ukuu wake. Christina katika albamu zake zote anataka kuonesha wa kumtegemea katika dunia hii inayoamini uwapo wa Mungu na manabii wake, ukiiangalia nyimbo zote utaona kwamba ni maombi kwa Mungu maombi ya kuonewa huruma na kusaidiwa kuona katika safari ya kufika mbinguni. mwisho

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Muziki wa Christina Shusho anavyofunza upendo wa kweli
Muziki wa Christina Shusho anavyofunza upendo wa kweli
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2021/10/muziki-wa-christina-shusho-anavyofunza.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2021/10/muziki-wa-christina-shusho-anavyofunza.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy