TITAN Sabmarini iliyoua mabilionea watano .Muundo wake wahisiwa kuwa chanzo cha kufumuka, hakikufuata mfumo .Inaelezwa kilishindwa k...
TITAN
Sabmarini
iliyoua mabilionea watano
.Muundo
wake wahisiwa kuwa chanzo cha kufumuka, hakikufuata mfumo
.Inaelezwa
kilishindwa kuhimili mgandamizo bahari ya Atlantiki
.Walikuwa
wanaenda kuzuru TITANIC walipofia matajiri wengine 1912
Na
Rahel Pallangyo
ILIKUWA
ni safari ya kwenda kwenye mabaki ya meli iliyozama kwa kasi mwaka 1912, safari
iliyotarajiwa kutumia kutumia saa 10 ndani ya sabmarini (nyambizi) Titan, iliyotengenezwa mahususi
kwa ajili ya mbizi za kina kirefu.
Titan
(iliyojulikana kama Cyclops 2 hadi 2018)
ni chombo cha pili cha kupiga mbizi kilichoundwa na OceanGate,
kinachomilikiwa na kampuni binafsi na kikiwa na uwezo uliokusudiwa wa
kufika mita 4,000 (futi 13,000).
Kikiwa
ni chombo cha kwanza cha chini cha maji kilichokamilishwa kikiwa kimejengwa na
titanium na nyenzo zenye mchanganyiko wa nyuzinyuzi za kaboni zikipitishiwa
metali zote muhimu kwa ajili ya kuhifadhi maisha ya binadamu.
Lakini
pamoja na tajiri yake kuamini kwamba
kazi ya kihandishi imefanyika vyema, wapo wataalamu waliowahi kutumia chombo
hicho wanasema kilikuwa na shida na hawakushangazwa na kufumuka kwake kulikotokana na kubanwa na
uzito mkubwa wa maji.
Ni kazi
kubwa kuamini na itachukua muda watu kupata majwabu sahihi nini kilitokea
katika nyambizi hiyo, lakini kauli za watu zinaonesha kwamba kulikuwa na
ukiukwaji wa taratibu za kiuhandisi.
"Unakumbukwa
kwa sheria unazovunja," anasema mmiliki na mmoja wa watu waliokufa, Stockton Rush akimnukuu Jenerali wa Marekani
Douglas MacArthur kuhusu nini amekifanya kuwa na Titan.
"Nimevunja
sheria kadhaa," anasema kuhusu Titan. "Nadhani nimezivunja kwa
mantiki lakini kuna uhandisi mzuri nyuma yangu uliowezesha chombo kujengwa na
kuwa salama." anasema Rush akizungumza na waandishi wa habari mwaka 2017
lakini Juni 18, 2023, OceanGate ilipoteza mawasiliano na Titan wakati wa kupiga
mbizi kwa mara ya kwanza mwaka huo kuelekea
kwenye meli ya Titanic.
Stockton
Rush III alizaliwa California mwaka 1962
katika familia ambayo ilitengeneza utajiri wake kutokana na mafuta na meli
anapenda sana kuvumbua na katika pilikapilika hizo amekufa.
Kwa
kuwa Titan ilikuwa inapoteza mawasiliano mara nyingi wakati wa majaribio ya
awali wa upigaji mbizi wa kitalii, OceanGate haikutahadharisha mamlaka kuhusu
kadhia hiyo hadi saa nyingi zilipopita bila chombo hicho kuibuka.
Juni 22, 2023 jeshi la Marekani
linaloshughulika na ulinzi wa pwani ya taifa hilo walipotoa taarifa kuhusu
kishindo cha kufumuka kwa chombo chini ya bahari nabaadaye kupata baki la chombo hicho kikiwa
katika omo la meli ya Titanic ambayo ndiyo ilikuwa inatembelewa.
Titanic
iliyozama mwaka 1912 imeteka fikira za umma, kwani idadi ya abiria na aina zao
ambao wengi walikuwa ni matajiri wa Ulaya waliotaka kuinjoi baharini na kufika
Marekani walikufa.
Kipindi
hicho Titanic ilikuwa moja ya meli kubwa na tajiri zaidi ulimwenguni. kama
waliokufa wakati huo ni amatajiri pia waliokufa safari hii ndani ya Titan nao
walikuwa matajiri akiwemo aliyebuni na
kutengeneza chombo chenyewe.
Titanic
ilijengwa kwa kuhakikisha kwamba haiwezi kuzama, kutokana na mfululizo
kihandisi ulioweka umadhubuti kiasi cha kufanywa kama upinde unaovutika.
Pamoja
na umahiri kwa kihandisi siku nne baada ya kuondoka bandarini 1912 meli hiyo
ilikwaa jabali la barafu ikakatika na kuza katika kipindi cha saa tatu tu,
hapakuwepo na muda wa kutosha kuokoa watu katika majira ambapo bahari ilikuwa
baridi zaidi.
Ni moja
ya misiba mikubwa ya dunia ya sasa. Ilizama muda huo lakini mabaki yake
yalikuja kuonekana mwaka wa 1985 ikiwa imeachana kivipande kwa umbali wa
kutosha.
Ikiwa
inapatikana 41°43′57′′ Kaskazini na
49°56′49′′ magharibi hapa ndipo Titan yenye watu watano wote matajiri
walipokuwa wamepanga kuzuru kiasi cha futi 13,000 sawa na mita 2000 kutoka
usawa wa bahari, kiasi cha takriban maili 400 za baharini (kilomita 740) kutoka
Newfoundland, Canada.
Tunaambiwa
vipande hivi viwili kuu omo na tezi yaani gubeti na shetri kwa maneno mengine
na hawa watalii sehemu ya mabaki ya
sabmarin yalionekana katika omo.
Katika
historia tunaambiwa kwamba omo la Titanic lilijikita katika usawawa sakafu ya
bahari saa nane na dakika 29 usiku. Lakini shetri inaelezwa ilijikita chini
dakika 27 baadaye ikishuka kutoka usawa wa bahari kwa kasi ya maili nne kwa
saa.
Vipande
hivi viwili vikiwa chini katika sakafu
ya bahari ikiwa ni futi takribani 13,000 vimejitenga kwa futi 2000 vikielekea
pande tofauti.
Inaonekana
Titan ikiwa na abiria wake watano inaonekana ilikaribia kufika kunakokusudiwa
yaani kiasi cha maili 2.4 kwenye sakafu
ya Bahari ya Atlantic kabla ya kuzidiwa na kufumuka.
Bahari
ya Atlantic ambayio ipo Kaskazini na Kusini mwa Marekani kwa upoande wa
Magharibi huku Ulaya na Afrika kwa upande wa mashariki inaungana na bahari ya
Arctic kw aupande wa kaskazini na kusini bahari ya Southern. Wanasayansi
wanagawa bahari ya Atlantic mara mbili yaani beseni la Kaskazini kama North
Atlantic na beseni la kusini kama South Atlantic.
Watalii
hawa sio tu walikuwa wanakumbana na hali isiyo kawaida kwa bahari kuu hii ya
pili kwa ukubwa duniani ambhayo hutengeneza mustakabali wa hali za hewa tofauti
na upigaji wa vimbunga visivyokuwa vya kawaida eneo hilo lenye pia pomboo na
kasa wa baharini.
Bahari
hii yenye zaidi ya maili za mraba milioni 41 ndio nyumbani kwa mabaki ya meli
kubwa duniani nyakati hizo ya Titanic baada ya kusakwa kwa miaka kadhaa Septemb
1, 1985 ikiwa imejitukliza katika futi 13,000 umbali wa mali za baharini
400 sawa na kilometa 740 kutoka Newfoundland, Canada. Mbaaki haya
ambayo omo ipo kwingine na shetri
kwingine ipo katika eneo la 41°43′57′′ kaskazini na 49°56′49′′ magharibi.
Kiukweli
baada ya kubainikwa Titanic imekaa eneo gani, watu walianza kuwania kiutalii na
pia kuitumia na mwaka 1997 James Cameron alitengeneza filamu ya Titanic.
Kampuni
ya OceanGate Inc. inayomilikuwa na
wamarekani mmoja ikiwa katika eneo la Everett, Washington, ndilo limetengeneza
nyambizi zinazotumika katika sekta ya utalii, viwanda, utafiti na uvumbuzi.
Kampuni hii ilianzishwa na watu wawili Stockton Rush na Guillermo Söhnlein
mwaka 2009
Walipoanza
walinunua nyambizi mbili na baadaye kuunda za kwao Cyclops 1 na 2 ambayo waliibatiza Titan. Mwaka 2021, OceanGate walianza kufanya
biashara ya utalii kuwapeleka watu kwenye mabaki ya Titanic kwa lengo la
utalii. Mwaka jana, 2022, bei ya mtalii mmoja katika safari ya OceanGate kuelekea
mabaki ya Titanic ilikuwa ni dola za Marekani 250,000 sawa na Sh 601,000,000 kwa mtu mmoja.
Juni
18, 2023 Titan iliua watu watano
waliokuwa wakielekea ikwenye mabaki ya Titanic akiwemo mmoja wa wamiliki Rush.
Timu ya waokoaji ya kimataifa ilibaini mabaki Juni 22, 2023 karibu kabisa na omo la Titanic.
Nani
ni Stockton Rush
Stockton
Rush anasema katika maihsa yake alipenda sana kukabili changamoto za anga za
juu na akiwa bado kijana miaka 18 alishakuwa na leseni ya urubani.
Akiwa
mkubwa alihamisha hamu zake hizo ikiwamo kuwa mtu wa kwanza kwenda Mars na
kujikita katika utafiti wa bahari. Rush alitengeneza utajii mkubwa baada ya
kuwekeza urithi wake katika kampuni za teknolojia ya kihandisi na kuamua kunua
sabmarini.
Katika
hekaheka hizo alibaini kwamba kusonga mbele kwa kuwa kulikuwa nasabmarini 100
tu zinaozmilikuwa na watu binafsi. Aliamua kutengeneza ya kwake wenyewe. Mwaka 2006 alitengeneza
Kittredge K-350 ambayo aliibatiza Suds.
Uzoefu
wa Rush na utafiti aliokuwa anaufanya alibaini kwamba kuna biashara kubwa
ambayo jamii bado kuishughulikia nayo utalii wa baharini kwa kutumia nyambizi.
Akajikita
katika kuangalia sheria na taratibu kisha tamaa ya kutalii kwenye sakafu ya
bahari, akabini akianzisha biashara hiyo hatakuwa na shaka , inalipa.
Kwa
kutumia vyombo vyake mwaka 1986 alianzisha utalii wa sakafu ya bahari kwa
kutumia sabmarini kupitia kampuni yake ya Atlantis Adventures ambapo watalii
walipelekwa katika kisiwa cha Grand Cayman . Mwaka 2003, zaidi ya watu milioni
2 walifanya utalii huo wa chini ya
bahari lakini eneo salama ambapo alijipatia dola za Marekani milioni 150 sawa na Sh 360,600,000,000.
Mwaka
2009-2013 Stockton Rush alifanya maendeleo makubwa katika biashara hizo ikiwamo
ya kuanzisha OceanGate akiwa na Guillermo Söhnlein huko Seattle mwaka 2009.
Kwa
mujibu wa Söhnlein,kampuni hiyo ilianzihwa kwa lengo la kuanzisha nyambizi
zinazoweza kubeba watu watano za kutosha ili kukodisha kwa watu na kampuni
binafsi.
Mwaka 2023 aliiambia Sky News kwamba wanatengeneza nyambizi kwa ajili ya kufungua
mipaka ya utalii katika sakafu ya bahari kwa binadamu wote.
Kampuni
hiyo nyambizi yake ya kwanza ilikuwa Antipodes, iliyokuwa imetumika na ilikuwa
na uwezo wa abiria watano .
Kati ya
mwaka 2010 na 2013 kampuni hiyo iliwezesha upigaji mbizi 130 wakitumia
Antipodes.
Kampuni
hiyo iliendesha shughuli hizo kwa kusafirisha watafiti, kukodisha na
kusafirisha watalii waliowaita wanasayansi wakazi.
Söhnlein
alikadiria kwamba mwaka 2012 abiria wato
walilipa kati ya Dola za Marekani 7,500 na dola 40,000 kwa kila mwanasayansi huyo ikitegemewa aina
ya safari.
OceanGate
ilitengeneza nyambizi yake Cyclops, ambayo waliita Cyclops 1 na kati ya mwaka
2016-2023 walifanya maendeleo makubwa japo mmoja wa waanzilishi alijitoa na
kubakiza hisa chache.
Mwaka 2019 OceanGate ilianza kujipanga kutengeneza
Cyclops 3 na Cyclops 4 lengo likiwa ni kuweza kufika mita 6,000
( sawa na futi 20,000) na mwaka 2021 OceanGate ilifanya jaribio lake la
kwanza la kuelekea katika mabaki ya meli ya Titanic ndani ya Titan.
Kifo
cha Rush huenda kikabadili mwelekeo wa
kampuni lakini tayari kuna shaka na jambo lenyewe.
Kuna
sababu ya mgandamizo
Titan unaweza kusema pasi shaka ilifumuliwa na
mgandamizo wa maji ambapo kwa kiingereza unaitwa "catastrophic
implosion"
na
kumuua Stockton Rush III ambaye kimsingi ni mwanaanga wa anga za juu na
rubani akiwa amefanyakazi na Shirika la
Utafiti wa Anga za juu (NASA).
Rush akiwa na mfanyakazi mwingine mwaka 2021
wakati wa majira ya kiangazi walifika katika mabaki ya Titanic.
James
Cameron amemshutumu mwanzilishi wa
chombo hicho kwa kuangalia zaidikibinafsi na kutioweka mmbele usalama.
David
Pogue, mwandishi wa CBS a,baye alikwenda katika safari ya 2021 na Rush
anasema Titan haikuwa imetengenezwa na
chuma cha kawaida bali na malighafi ambazo hazijajaribiwa kuhimili mgandamizo
wa maji.
Rob
McCallum,m,vumbizi ambaye pia alikuwa mshauri OceanGate, aliwahi kumweleza Rush
aachane na kubadilisha msingi wa kawaida wa uumbaji wa nyambizi na kuwa na
urahisi inapogusa kwenye kina cha
Titanic.
Katika
email kwa Rush, Machi 2018, McCallum alisema: "Unataka kutumia teknolojia
isiyo ya kiwango katika sehemu yenye changamoto sana ya mgandamizo. Kadiri
ninavyothamini suala la ujasiriamali na
uvumbuzi, kitendo chako kinaweza kuweka tasnia nzima matatani.
"Kupeleka
chombo chini katika kina cha mita 4,000
katikati ya Atlantiki sio mchezo hapo si mahali unapoweza kukata kona."
Rush, hakujibu vyema alisema kwamba amechoshwa
nna watu wanaozuia uvumbuzi kwa hoja ya kuangalia usalama kwanza.
Usalama
ulikuwa "kuhusu utamaduni, sio makaratasi", alisema. Alizungumza juu
ya kuhitaji "muundo wa busara, majaribio ya kina, na idhini ya washiriki",
lakini akasema kipande cha karatasi hakikuhakikishia usalama wa sehemu ndogo.
Miezi
kadhaa iliyopita mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa OceanGate ,David Lochridge
alisema kwamba kuna vitu vibngi ambavyo vilionekana kuwa tishio kwa usalama wa
nyambizi hiyo.
Mwaka
2018, Jamii ya Marine Technology Society
aliiandikia OceanGate ikituhumu madai yasiyokuwa na ukweli ya usalama wa
nyambizi hiyo.
Mgandamizi
mkubwa unaamini kwamba ulisababisha chombo hicho kuvunjika vipande vipande na
kusababisha maafa kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa OceanGate CEO Stockton Rush,
61;veterani wa Kikosi cha maji cha Ufaransa Paul-Henri (PH) Nargeolet, 77;
bilionea kwa Kiingereza Hamish Harding, 58; Mfanyabiashara wa Pakistan Shahzada
Dawood, 41; na mtoto wake mwenye umri wa
miaka 19 Suleman.
Kufumuka
kwa sabmarini hiyo kumeelezwa kuwa kumetokana napresha ya ndani kuwa ndogo
zaidi kuliko mgandamizo wa nje
Wakati
chombo aina ya nyambizi kinaingia chini baharini kinachofanyia ni kuwa presha
ya ndani ni kubwa zaidi kuliko mazingira, au maji yaliyopo nje ya chombo.
Inaaminika
kwambaTitan ilizidiwa na kiasi cha mgandamizi unaofikia pauni 5,500 na 6,000
kwa inchi moja ya mraba. Huu ni mgandamizi mkubwa kwani ukilinganisha na
shinikizo la angahewa kwenye usawa wa bahari la pauni 14.7 kwa kila inchi ya
mraba.
Ingawa
bado haijafahamika ni nini hasa
kilitokea na kusababisha Titan kuharibika, kuna uwezekano kuwa kuna kitu
kilisababisha kuvuja kwa mgandamizo wa ndani na hivyo kutoa nguvu kubwa kwa
mgandamizo wa ndani.
Roderick
Smith, profesa wa uhandisi katika Chuo cha Imperial London, anasema kwamba
uwezekano huo ulitokana na "kushindwa kwa shinikizo la ndani eneo la omo
" lakini hii haitajulikna mpaka
mabaki yote yawe yamekusanywa na kuangaliwa sababu.
Hata
hivyo Smith anasema kwamba jinsi mfumo huo ulivyokuwa kutakuwa na shida kubwa
kuweza kumaizi sababu.
Kiukweli anasema Smith ili chombo kiweze kuwa
salama katika kina kirefu kinahitaji kuwa na
umbo ambalo huruhusu kustahimili shinikizo sawa kwa pande zote.
Aileen
Maria Marty, mwanamaji wa jeshi la Marekani mstaafu anasema kwamba mgandamizo
hufumua chombo katika sekunde nchache sana.
"Jambo
lote hutukia hata kabla ya watu walio ndani hata kugundua kuwa kuna
shida."
Dk Dale Molé anaamini kwamba tukio lillitokea
haraka kiasi ya kwamba hata abiria wenyewe hawakujua nini kimewapiga.
mwisho
Makala haya yaliytolewa kwa mara ya kwanza na HABARILEO
COMMENTS