MAJESTIC CINEMA :JENGO KONGWE LINALOENDELEA KUONESHA SINEMA

Na Rahel Pallangyo  WAKATI wa safari yangu ya Tanga hivi karibuni katika michuano ya Ngao ya Jamii kwenda kuandika habari na kupiga picha za...


Na Rahel Pallangyo 

WAKATI wa safari yangu ya Tanga hivi karibuni katika michuano ya Ngao ya Jamii kwenda kuandika habari na kupiga picha za michezo, nilipita karibu kabisa na jumba la sinema la Majestic lililopo barabara ya Mkwakwani.



Jumba hilo la Shirika la Nyumba (NHC) ni la zamani na mpaka sasa linaendelea kuonesha filamu na kufanya kazi nyingine za burudani. Ikumbukwe kuwa ka tika miaka ya 1980 ambako kulikuwa na mdororo wa kiuchumi hamu ya kwenda sinema ilipungua kutokana na majumba hayo kutokuwa na bidhaa mpya inayovu tia wakawa wanababia na kuchosha wapenzi wa sinema. 

Katika jengo hilo Tanga wapenzi wa sinema wa naopenda kuona vitu hivyo katika ‘Big Screen’ walipo teza burudani hiyo kutokana na kufungwa kwa majumba ya sinema ambayo yalikuwa na uwezo wa kuonesha mm 35 bado wanaendelea kuona kwa kutumia jengo lao am balo ujenzi wake ni urithi safi wenye kumbukumbu. 

Ingawa wapenzi wa bu rudani hiyo kabla ya miaka ya 1980 hawakuweza kufikiri hata mara moja kwamba kutakuwa na kufungwa kwa majumba ya sinema ukiz ingatia wananchi walikuwa wanafurika kuona sinema za kidosi au za kizungu. 

Mathalani Dar es Salaam majumba yote yaliyokuwa yakionesha filamu kama Drive in, Empire, Avalon, Empress, Odeon, Cameo, New Chox na Star Light yamegeuka kuwa majumba ya kazi nyingine na mpaka kesho inaonekana haiweze kani tena kurejea katika mazingira ya zamani.

 Ukiachia Dar es Salaam mji wenye starehe za kipekee wa Morogoro ulikuwa na Shani Cinema na Sapna. Vivyo hivyo katika Mkoa wa Lindi ambapo pale penye ukumbi unaoitwa Y2K kulikuwa na jengo kubwa la filamu. Mpaka mwishoni mwa miaka ya 1990 ilikuwa ni ada kutafuta magazeti kuona nini kinaendelea katika majumba ya sinema ya Dar es Salaam na hata huko mikoani katika mbao za matangazo ya ma jumba hayo. 



Ingawa majumba mengi yamekuwa nyumba za ibada, maduka au yamefungwa au kubomolewa na majengo mengine kusimamishwa badala yake, Tanga wame onesha kwamba Majestic yao ambayo ilitumika kuonesha filamu ya kwanza huru, Shamba Kubwa, inaweza kuendelea kuwapo. 

Majestic Theatre haikuwa peke yake katika mji huu am bao kuingia ni rahisi na ku toka ni kazi kwani kulikuwa na Regal, Novelty na Tanga Cinema lakini leo hii unaona kwamba Majestic ndio wa meendelea kuwapo mpaka kesho na bado wanaonesha inawezekana kuendelea kuonesha filamu.

 Historia inasema katika Jiji hilo jengo la kwanza kufa ni Tanga cinema, ikafuata Novelty, Regal na mwisho Majestic ambao kwa sasa wamefufuka. 

Nilipata nafasi ya kuzun gumza na mmoja wa walimu wa sanaa ya filamu, Profesa Martin Mhando kuhusiana na jengo la Tanga na kunia mbia ndilo lililotumika kuon esha filamu ya kwanza huru ya Shamba Kubwa ambayo pia ploti yake ilikuwa Mkoa wa Tanga. 



Aliniambia ingawa Majes tic ya Tanga haina uhusiano na jengo la jina kama hilo Zanzibar ambalo lilipiganiwa kuimarishwa na kuendelea na kazi yake ya kuonesha filamu, anaamini utamaduni wa kuona sinema unarejea kutokana na juhudi mbalim bali za watengeneza filamu hapa nchini na duniani kwa ujumla.

 Shamba Kubwa moja ya filamu zilizoanzisha tena utengenezaji wa filamu Tan zania baada ya kampuni ya filamu kufa na filamu zake kubaki Zimbabwe zilipoenda kwa ‘treatment’. Shamba Kubwa sinema ya mwaka 1994 ilimtambulisha Jimmy Mponda kama J. Plus wengine wakimuita Jimmy Master ilipata jina kubwa na pia kuleta vuguvugu mpya ya matamanio ya burudani kupitia majumba ya sinema.

 “Majestic Theatre ya Tanga naijua kama moja ya majumba ambayo yalibaki kuonesha filamu kwa muda mrefu wakati majumba mengine yalipokufa kabisa Tanzania. Mwaka 1995 ilipo tengenezwa Bongo Movie ya kwanza iliyoitwa “Shamba Kubwa” na Amri Bawji na Kassim El Siagi, filamu hiyo ilioneshwa Majestic, Tanga,” anasema Profesa Mhando na kusema kuwa hali iliyokuta majumba ya sinema nchini Tanzania Bara na Visiwani matokeo ya mdororo wa kiuchumi. 

“Uchumi ulidorora miaka ya 1980,” Mhando alisema. “Tiketi zilikuwa zimegharimu dola za Marekani 1-2, lakini tulijua ikifika dola 3 uchumi wa sinema utaporomoka na ndivyo ilivyokuwa. Watu hawakuwa na uwezo wa kutazama sinema. Video zili kuja na kukaa ndani. Kufikia 1996, sinema zote zilikuwa zimefungwa.” 



Anasema ingawa hana uhakika kuwa Majestic ya Tanga na Majestic Zanzibar zilihusiana ingawa inawezekana, maana waliokuwa wa nahodhi majumba ya sinema walikuwa Watanzania wenye asili ya India, kuendelea kuwepo kwa jengo hilo likiendelea na kazi ya kuleta burudani inatia matumaini si tu kwa urithi wa kizazi kijacho bali na uhakika wa maeneo ya kuonesha uwezo wa binadamu katika skrini kubwa. 

Anasema alikuwa anapigania sana Majestic ya Zanzibar na anafikiria safari ni nzuri kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ime kuwa tayari kulifufua Jumba la Majestic kwa kupata misaada ya kimataifa. “Mimi nimekuwa nikip igia kelele na kuliwekea kifua ili lisibadilishiwe matumizi kama majumba mengine. Kwa sasa jumba hilo limetolewa kwa Muungano wa taasisi tano kusimamia ukarabati na kulipa matumizi mengi zaidi,” anasema Pro fesa huyo ambaye amebobea katika filamu. 

Taasisi hizo tano ni ZIFF, Hifadhi, Sauti za Busara, Women Reclaim Center na Abdul Mawazo. Anasema Unesco imesaidia kupata kia si cha fedha toka serikali ya Japan ili kufanya upembuzi yakinifu na kuanza mipango ya kukarabati jumba hilo. Ingawa kuna utata katika uhodhi/umiliki wa jumba le nyewe maana nalo lilitaifish wa wakati wa mapinduzi na sasa familia iliyokuwa inali miliki imerudi tena ili kutaka kuliendesha, mazungumzo yanaendelea kuhusu umiliki na hivyo kazi ya upembuzi imesimama. Unesco ndiyo inasimamia ukarabati.

 Hekaheka za kurejesha jumba hilo la Zanzibar linaenda na ukweli kuwa majumba ya sinema ka tika miaka ijayo ni muhimu katika kuhakikisha ukuaji mzuri wa tasnia kwani hata Ulaya walikoendelea bado majumba ya sinema yanafan yakazi hasa kuwezesha pato la kwanza katika kuingia katika majukwaa mengine. Majestic ya Zanzibar ni moja ya majumba ya kwanza ya sinema barani Afrika, katika miaka ya 1920. Zanzibar ilikuwa na majengo ya sinema 53 yakajifia na kubaki mawili likiwemo hilo la Majestic.

 Mtengenezaji wa filamu Mwingereza Nick Broom field, anayejulikana kwa filamu za Biggie na Tupac, Aileen Wuornos: The Selling of a Serial Killer na Battle For Haditha anafurahishwa na juhudi za kurejeshwa kwa majumba ya sinema. 

Akizungumzia jumba la Zanzibar ambalo halina paa kwa sasa watu wakiangalia sinema wazi alisema: “In gawa sinema haina paa, watu wanaitumia na kuweka pro jekta yao wenyewe. Pengine ina kumbukumbu nyingi kwao. Ni mahali ambapo watu walienda kwa kustare he na kukutana na rafiki zao wa kike wa kwanza. 

“Sinema ni uzoefu wa pamoja. Kama mtengenezaji wa filamu, jambo la ajabu zaidi kuhusu kutazama na kikundi cha watu ni kwamba unaweza kujua ni sehemu gani za filamu zinafanya kazi na zipi hazifanyi kazi.

 “Ni jambo la kuungani sha, njia ya kufanya kikundi au eneo pamoja. Nilipokuwa mdogo, kila mtu alienda kwenye sinema Jumamosi asubuhi ili kuona katuni. Ilikuwa ni ushirikiano wa kijamii, na hiyo ni moja ya mambo ya kusisimua am bayo yanaweza kutokea.

 “ Broomfield anasema: “The Majestic ni kipande cha usa nifu wa ajabu ... Kwa upande wa jumuiya ya watengenezaji filamu wa Afrika Mashariki, umuhimu wa Zanzibar ungewekwa katika kufufua Majestic. Ingekuwa faraja kwa watu kuchukua sinema kwa uzito. Pia itakuwa vy ema kwa tamasha la filamu la Kimataifa la Zanzibar.” 

“Nadhani ikiwa inger ekebishwa ipasavyo, watu wangeweza kwenda kwenye sinema huko mara kwa mara. Bado ina mapambo mazuri ya sanaa.” 

Mmoja wa wapenzi wa sinema Beda Msimbe anas ema ana tumaini kizazi kipya kikionja ladha ya kuingia majumba makubwa na uta maduni wake wataona raha. 

“Wazee bado wana ndoto zao za kutazama sinema kila wiki, wanakumbuka utukufu wa zamani wa majumba haya na enzi za ujana wao. Huo ndio umuhimu wa uta maduni wa sinema kwao.

” Majestic ya Tanga hivi karibuni ilionesha filamu ya kisayansi ya Eonii na mhudu mu wa jumba hilo anasema walijaza watu wa rika zote na kutamani hali hiyo kuendelea kuwa hivyo.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MAJESTIC CINEMA :JENGO KONGWE LINALOENDELEA KUONESHA SINEMA
MAJESTIC CINEMA :JENGO KONGWE LINALOENDELEA KUONESHA SINEMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipjmEHej8zI37SIdtgsESh6DS0qqYyvwE0mRA0kTWC1rNseFVu5aSfwNNXLAqENq0_sHZmyuB_xHgNnDG5Tj7N7Ov0f5oCPXlgKI9rUrVWwQibFud-KXQOiafKxse6XcUj8vzBzovECjJOdiYDGyvTYc3LdMlte0hY4GjFSEcztMXuFDNI3I63v6Gh6-QM/s320/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipjmEHej8zI37SIdtgsESh6DS0qqYyvwE0mRA0kTWC1rNseFVu5aSfwNNXLAqENq0_sHZmyuB_xHgNnDG5Tj7N7Ov0f5oCPXlgKI9rUrVWwQibFud-KXQOiafKxse6XcUj8vzBzovECjJOdiYDGyvTYc3LdMlte0hY4GjFSEcztMXuFDNI3I63v6Gh6-QM/s72-c/1.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2023/08/majestic-cinema-jengo-kongwe.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2023/08/majestic-cinema-jengo-kongwe.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy