Tiba kwa mfumo wa bima hulea taifa imara

Na Beda Msimbe ILI kuwepo na utaratibu mzuri wa afya duniani, wataalamu walibuni matumizi ya bima ambapo mtu huchangia mapema na kisha kup...

Na Beda Msimbe ILI kuwepo na utaratibu mzuri wa afya duniani, wataalamu walibuni matumizi ya bima ambapo mtu huchangia mapema na kisha kupata ahueni kwa shida ya tiba anapokumbwa na madhila ya maradhi. Ni kutokana na ukweli huo, nchi nyingi duniani zimeona umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa wananchi wake ili kila mmoja apate afueni anapopata na madhila ya maradhi. Suala hili la kuwa na bima ya afya Tanzania halikuanza jana, lilianza baada ya kupata uhuru wakati Israel ilipoombwa kuangalia namna bora ya kusaidia wananchi wa Tanganyika kupata huduma za tiba. Ilikuwa ni Julai 20, 1962 miezi saba baada ya kupatikana Uhuru kamili (Desemba 9,1961), Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje walitaka msaada wa kiufundi kutoka Israel kuhusu mpango wa bima ya afya kwa waajiriwa. Mtaalamu kutoka Israel alifanya kazi hiyo Oktoba 1962 na kuja na majibu ambayo yalionesha uwezekano wa kuanzishwa kwa mpango huo. Pamoja na mapendekezo mpango haukuanzishwa na mwaka 1967 wakati wa kutangazwa kwa Azimio la Arusha ilielezwa wazi kwamba wananchi wa Tanzania watapata huduma za afya na elimu bure. Hiyo ilikuwa ni sera ambayo iliungana na sera ya vijiji vya ujamaa ya mwaka 1974 hivyo kufanya huduma za afya kutolewa bure na hivyo kwa miaka 40 mfumo wa bima ya afya nchini haukutekelezwa. lionekana wazi kwamba serikali imezidiwa na sera mpya zikaundwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika sekta ya afya na elimu na ndipo mwaka 1995 Serikali ya Uingereza iliombwa kuangalia uwezekano wa kuanzishwa bima ya afya ambapo wanachama wake wataingia kwa mujibu wa sheria. Kitabu cha A historical Development of the National health Insurance Fund of Tanzania (2011) kimeelezea kwa undani zaidi nini kilijiri tangu wakati wa ukoloni hadi wazo la kuwa na bima ya afya mwaka 1962 na serikali kuamua kuwa na huduma bure hadi ilipoanza kubadili sera miaka ya 1990. Tangu awali dhana ya bima ya afya iliangaliwa kwa namna tofauti huku historia na utamaduni ukiathiri maelezo mengi ya kiufundi kutoka katika mataifa ambayo yana mifumo mbalimbali ya bima ya afya. Kimsingi bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwananchi ambaye anakuwa mwanachama kugharamiwa katika kupata huduma za kiafya zikiwemo za kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa. Kwa upande fulani bima ya afya ni kama mkataba unaoingizwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa wahuduma husika. Kwa sasa inatambulika zaidi kwamba bima ya afya huchukuliwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake na pia mwajiriwa mwenyewe. Hapa nchini pamoja na kuundwa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, pia zipo Bima zinazohusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao. Mara nyingi wanachama huchagua taasisi ama mifuko inayotoa bima kulingana na aina, viwango na mipaka ya taasisi hizo au bima hizo. Pamoja na kuwa na makampuni ya bima kama Strategies, AAR na nyinginezo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ndio bima inayozungumzwa sana kwa kuwa imebeba wanachama wengi na hasa baada ya kuunganishwa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mwanzo wa bima Tanzania Kutokana na mageuzi ya sera ya sekta ya afya 1993 serikali iliangalia namna nzuri ya kuhudumia wananchi wake, mwaka 1999 serikali ilianzia NHIF kama taasisi ya umma chini ya sheria namba 8 ya mwaka 1999 (sura ya 395 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) Mfumo wa uchangiaji unategemea kundi la huduma na pia uwezo wa kulipa wa mwanachama na si vinginevyo. Kwa mujibu wa sheria ya NHIF wafanyakazi na waajiriwa katuika sekta ya umma wana wajibu wa kujiandikisha na kuchangia asilimia sita ya mishahara yao ya kila mwezi. Pamoja na mambo mengine, utaratibu wa waajiriwa ambao upo kwa mujibu wa sheria wigo umepanuka zaidi kwa sasa na kuingiza makundi mengine kama wanafunzi, watoto, viongozi wa dini, mama lishe na kadhalika. Kwani muhimu kujiunga na bima Kuna sababu nyingi zinazozungumzwa lakini kubwa zaidi kwa mujibu wa Basil Msongo, Mhariri wa Habari wa HabariLeo ni mkombozi wa dharura. Bima husaidia sana mambo ya ghafla wakati huna fedha taslimu na wakati mwingine ukiwa mgonjwa ghafla na huku ukiwa na kitambulisho chako cha kadi ya uanachama. Mwanachama wa NHIF anayekaa Magomeni Usalama, Maulid Ahmed anasema kwamba Bima ya Afya imemsaidia sana kutokana na matatizo ambayo anayo kama kisukari ambapo huchukua dawa kila mwezi na vifaa vya kupima sukari nyumbani. Na pamoja na dawa anazochukua kila mwezi, kabla ya ugonjwa huo ameshafanyiwa operesheni kwa kutumia kadi ya NHIF. “Naishi kwa amani, najua nikiumwa wakati wowote sihitaji hela kwa matibabu kwa kuwa nina bima,” anasema Maulid. Pamoja na manufaa yake anasema kuna haja ya kuangalia sheria upya ya ushiriki wa bima hiyo, kutosubiri muda mrefu kabla ya kuanza kupata matibabu na pia kuhamishwa kwa akaunti ikiwa mwenye akaunti amekufa wakati ndio kwanza kalipia bima tena kwa fedha ndefu. Alfred Lasteck anayeishi Kimara akizungumzia faida za bima anasema: “Kimsingi nimepunguza gharama za matibabu. Pia nimeweza kusaidia wengine kutoniomba huduma za matibabu.” Kwa hatua yake ya kuchukua bima anasema amesaidia watu wengine, mkewe na watoto na wategemezi ambao wananufaika na matibabu na huduma nyingine za bima zinazotolewa na NHIF. Oliva Kibua anayekaa Mbezi Malamba Mawili akizungumza akiwa katika kituo cha afya Kimara anasema kwamba yeye hana bima ya afya kwake na mtoto wake, na anapata shida sana mtoto wake au yeye mwenyewe anapougua. Kutojiunga kwake na bima ya afya anasema kunatokana kutokuwa na fedha. Anapoulizwa kama anajua kwamba kuna bidhaa nyingi (huduma) katika mfuko anasema hajui na haelewi apate hizo habari wapi. Tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama Rwanda na Kenya, Watanzania wengi hawana huduma ya bima na wengi hawafahamu faida za kuwa na utaratibu wa bima. Ingawa Watanzania walio wengi (iwe mijini au vijijini), hawana huduma za bima, lakini walio na kipato kidogo hutaabika zaidi kunapotokea kadhia kubwa katika familia huku wakiwa hawana Bima. Familia hizi zenye kipato kidogo au kisichokuwa na uhakika hutumia akiba yao yote, kuuza mali au mashamba yao, kukopa kwa marafiki, au hata kukopa mahali ambapo wanatozwa riba kubwa sana ili kusaidia kukabiliana na ugonjwa ulioingia katika familia hiyo. Takwimu zilizopo zinaonesha kwamba asilimia 92 ya Watanzania hawana huduma yoyote ya bima huku wenye bima rasmi wakiwa asilimia 6.4 na isiyo rasmi asilimia 1.9. Hii ni kwa mujibu wa FSDT/Finscope Survey ya mwaka 2009. Pia, utafiti uliofanywa mwaka 2009 na The First Microinsurance Agency Limited iliyopo Dar es Salaam iliyohusisha watu 600 na ikifanywa na kundi la Steadman ulionesha kuwa walio wengi wanapendelea kuwa na bima ya Afya. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao unasimamia pia huduma kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ina jumla ya walengwa 10,206,980 ambayo ni sawa na asilimia 23.46 ya Watanzania wote. Kufikia Desemba 2019, wanachama wa NHIF walikuwa 4,856,062, sawa na asilimia 9 ya watanzania. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya, Mama Anne Makinda amekuwa akisisitiza watanzania kujiunga na mpango wa bima ya afya ambao ndio mfumo bora wa afya duniani kote. Kukiwa na zaidi ya vituo 7,000 vilivyosajiliwa na NHIF kwa Tanzania nzima kuanzia zahanati, hospitali za mikoa, kanda na Taifa, Mwanachama wa NHIF ananufaika na mambo zaidi ya 10. Meneja mawasiliano wa NHIF, Angela Mziray anasema mwanachama wa NHIF kwanza ananufaika na ada ya kujiandikisha na kumwona daktari, huduma ya dawa, huduma za vipimo, huduma za wagonjwa wa nje na kulazwa na huduma za upasuaji mdogo, mkubwa na wa kitaalamu. Anataja manufaa mengine kuwa ni kupewa huduma ya tiba ya kinywa na meno, huduma ya tiba ya macho, huduma za miwani ya kusomea kwa mwanachama mchangiaji, huduma za mazoezi ya kimatibabu ya viungo, matibabu kwa wanachama wastaafu na wenza wao bila kuendelea kuchangia, kwa wale wanachama waliokuwa wanachama kupitia ajira zao na kupatiwa vifaa tiba saidizi kama vile fimbo nyeupe, magongo ya kutembelea na vifaa vya usikivu.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Tiba kwa mfumo wa bima hulea taifa imara
Tiba kwa mfumo wa bima hulea taifa imara
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9vjvmhFQwE97jOpckD_w54alyh8QoFKkTxDvUNQH1B4846R-D6E_LUXI0st16ACko7BVoHAbtB8N8faKII67r84uyvNupev8YUOT4auBmocpU-9PXnarKSGdbRdRw2FrxMoJRuPzb7q_789fCr8ziWatZQKtFQtijG20ynVq1Vfi0oZFTQLggfxbtZk9j/s320/matibabu.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9vjvmhFQwE97jOpckD_w54alyh8QoFKkTxDvUNQH1B4846R-D6E_LUXI0st16ACko7BVoHAbtB8N8faKII67r84uyvNupev8YUOT4auBmocpU-9PXnarKSGdbRdRw2FrxMoJRuPzb7q_789fCr8ziWatZQKtFQtijG20ynVq1Vfi0oZFTQLggfxbtZk9j/s72-c/matibabu.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2024/01/tiba-kwa-mfumo-wa-bima-hulea-taifa-imara.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2024/01/tiba-kwa-mfumo-wa-bima-hulea-taifa-imara.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy