UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI Shughuli nyingi zinazofanywa na serikali zinaweza kuleta msisimko mkubwa kwa wananchi na kujifunga ni...
UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI
Shughuli nyingi zinazofanywa na
serikali zinaweza kuleta msisimko mkubwa kwa wananchi na kujifunga nira
ya maendeleo katika maeneo yao kama shughuli hizo zitakuwa zikitangazwa.
Utoaji wa habari iwe katika mfumo wa
magazeti au kielektroniki kama televisheni na radio na mitandao ya kijamiii
husaidia kutawanya habari na mara zote habari hizo huleta athari katika
jamii inaweza kuwa chanya au hasi.
Mara nyingi taarifa hizo huwa ni
habari njema kwa makundi mengi kwa kuwa huleta ushawishi unaoweza kung’amuliwa
na wengine na kufanyiwa kazi kupata athari inayohitajika.
Kama watu watajua umefanya nini na
umefanikiwa nini na nini unakifanya kwa sasa, mara nyingi unaweza kupata ama
kuigwa au mtu mwingine akakupata msaada pale ambapo anaona unafanya kitu chema
laini unakabailiwa na changamoto katika kitu hicho.
Wakati ni muhimu sana pia
kutotumia vyombo vya habari kujifaharisha badala ya kuonesha kazi
inayohusika, matumizi ya vyomboi vya habari kwa usahihi huweza kuleta
mabadiliko yanayokusudiwa.
Sasa labda nieleze kwanini
vyombo vya habari ni muhimu kwa serikali.
kwa nini vyombo vya habari ni muhimu
Kimsingi umuhimu wake unatokana na
ukweli kuwa vina uwezo wa kupeleka ujumbe wa kitu unachofanya au unachohitaji
kwa watu wengi kwa mkupuo mmoja.
Kuna aina nyingi ya vyombo vya
habari ingawa wengi tunajua uwapo wa televisheni, radio na magazeti. Vyombo
hivi hus
aidia kukusanya na kutawanya habari yakiwamo matukio mbalimbali. Lakini
siku hizi pia kuna mitandao ya jamii kama blogs,facebook, twita na kadhalika.
Ukifanikiwa kufikisha ujumbe wako katika vyombo vya habari maana yake katika
muda mfupi sana watu wanajua kinafanyika nini. Kwanini kinafanyika na nini hasa
faida kwa watu wa eneo husika.
Kwa kukosa vyombo vya habari maana
yake kinachofanyika katika eneo lako, hakuna mtu atakayejua. Na kama hajui
uwapo wa mavuno mengi yanayotafuta soko, Yule mwenye shida ya mavuno hayo
hatajua kwamba anatakiwa kufika kwako. Kama eneo linafikika na wewe hujatangaza
kwamba eneo hilo lina mathalani mpunga na linafikika nani atajua. Katika
ulimwengu wa utandawazi vyombo vya habari vinafikisha masuala kama haya
kwa haraka na wengine wakisoma au kuangalia wanakubaliana nayo.
Kimsingi hakuna kitu kianchoweza
kujulikana kwa kasi na kwa spidi inayotakiwa bila kutumia vyombo vya habari.
Husaidia kufikisha ujumbe kwa watu unaowataka
Husaidia kufikisha ujumbe kwa watu unaowataka
Kuna aina mbalimbali za vyombo vya
habari. Na kama ukiangalia vyombo vinavyotakiwa maana yake unaweza kujua chombo
gani kitafikisha nini na kwa watu wa naina gani kwa mfumo gani.
Kuna vyombo vya habari vinavyotumika
sana na vijana na kama unaweza kutumia vyombo hivi maana yake unaweza
kuwasiliana na vijana moja kwa moja.
Unaweza kuangalia ukubwa wa eneo na
nanin anastahili kufikishiwa ujumbe siku hizi kuna radio za jamii, magazeti ya
maeneo na hata televisheni za halmashauri kwa ukubwa wa eneo halmashauri hizi
zipo poa kutumia kwa malengo ya ndani lakini kuvuka halmashauri vyombo vikubwa
zaidi vya kitaifa vinastahili kuangaliwa.
Na kubwa zaidi ni matumizi ya
intaneti ambako humo ndiko unakuta mitandao ya kijamii.
Tunzo kubwa ya vyombo vya habari ni
kwamba inakusaidia kutawanya habari, kupata taarifa na hata matangazo
mbalimbali yanayohusu mambo mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Moja ya faida kubwa unayoweza kuipata
kwa kualika vyombo vya habari katika eneo lako la kazi ni huduma ambayo ni bure
kwa watu wako na jamii yako.
Vyombo hivi ukiachia matangazo unayolipia
taarifa zinazogusa maisha ya watu na maendeleo yao hutoplewa bure kwa jinsi
ambavyo inafaa kwa namna ambavyo zinafaa kuwa habari kwa watu kama katika
muundo wa makala za maendeleo.
Na wanapokuwapo wawakilishi wa
vyombo vya habari unahakika kama kitu chako kitawafikia wengi zaidi.
Kitu cha msingi ingawa habari huwa
hazilipiwi, kama kusipokuwa na juhudi binafsi ya kutengeneza mawasiliano mema
na vyombo vya habari,kuandaa taarifa au matukio hayo na kuwa tayari kuzungumza
nao huwezi kufanikiwa.
Ni muhimu kuelewa kwamba kama
usipotia nia katika uhusiano mwema huwezi kufanikiwa kuwa na tarifa za bure
katika vyombo hivyo.
Pia utambue kwamba kwa
kuanika taarifa zako, shughuli zinazofanyika zitaonekana kuwa si za kimagumashi
ni za kweli na kwamba zinakujengea wewe na watu wako heshima katika ujenzi wa
taifa.
Na hii utambue ukweli kuwa watu
wanaamini kwamba kitu kinapotokea katika chombo cha habari ni cha kweli na
muhimu kuonwa au kusomwa.
Ni ukweli kuwa wengi wa wananchi
hutoa uzito mkubwa kwa habari ambazo zimeandikwa na kutoka katika vyombo vya
habari.
Kitu kingine ni vyema kutambua kwamba kwa kutumia vyombo vya habari unaleta mvuto katika eneo lako, wengi wawekezaji au watoa huduma hutafuta taarifa kwa namna ya kusoma au kuangalia vyombo vya habari nini wanachoweza kukifanya.
Kitu kingine ni vyema kutambua kwamba kwa kutumia vyombo vya habari unaleta mvuto katika eneo lako, wengi wawekezaji au watoa huduma hutafuta taarifa kwa namna ya kusoma au kuangalia vyombo vya habari nini wanachoweza kukifanya.
Kwa kuwa karibu na vyombo vya habari
unatengeneza mustakabali wa kueleweka kwa wewe na jamii unayoiongoza.
Pia inawezesha eneo lako
kujulikana vyema miongoni mwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Kuwapo kwa taarifa zako kila mara kunafanya watu waangalie eneo lako kwa namna tofauti.
Kwa kujulikana unaweza kushawishi aina mbalimbali za watu kufika kufanyakazi za kijamii au kiuchumi.
Kuwapo kwa taarifa zako kila mara kunafanya watu waangalie eneo lako kwa namna tofauti.
Kwa kujulikana unaweza kushawishi aina mbalimbali za watu kufika kufanyakazi za kijamii au kiuchumi.
LAKINI VYOMBO HIVI HIVI VINAWEZA
KULETA SHIDA
Kutokana na nguvu kubwa
iliyonayo ya kubadili mawazo ya watu vyombo hivi vinaweza pia kusababisha
sokomoko na hata kuzuia maendeleo.
Ni vyema kuwa makini katika hili na
hasa kutengeneza uhusiano mwema na pia kuwa tayari kuzungumzia changamoto
mbalimbali na pengine hata kabla wao wenyewe hawajauliza.
Unaweza kusema maoni yako namna
changamoto zinavyoweza kushughulikiwa na kwa nguvu ile ile ikatumika kushawishi
ushiriki wa kutatua changamoto hizo.
Tunataka ufahamu kwamba mawazo
mazuri yanayojenga yanaweza kubomolewa na mawazo mabaya yanayotengenezwa kwa
namna ambavyo yanasaidia kubomoa badala ya kujenga.
Maana yake ni kwamba jiandae pia
kukabiliana na habari mbaya kwa kuwa na mpango kazi unaoelekeza namna njema ya
kukabiliana na habari hizi na kuzigeuza changamoto zinazoweza kuonwa kama
changamoto na kusaidiwa kuondokana nazo badala ya kukutumbukiza katika siasa za
maji taka.
Kunatokea nini Tanzania
Wengi wa viongozi wanashindwa
kueleza mafanikio ya serikali katika nyanja mbalimbali kwa namna inavyofaa. Kwa
mfano ujenzi wa barabara nini faida yake kwa wale waliopembezoni na imeleta
muingiliano gani wa kiuchumi.
Mafanikio ya serikali ni mengi
lakini hakuna maelezo yanayozingatia nini kimefanyika, kimesaidia nini.
Vyombo vya habari vya Tanzania
vinatumika zaidi kueleza mabaya ya watumishi wa serikali na hivyo serikali
kuonekana kuwa mbaya. Viongozi wanashindwa kujieleza katika masuala ambayo
yanaweza kusaidia kuonesha serikali inafanya nini.
Viongozi wamekuwa wavivu hata
kutumia magazeti ya serikali kuelezea mafanikio kwa lugha nzuri tu. Kushawishi
maeneo kuonesha maendeleo yaliyotokana na sera nzuri za serikali.
Viongozi wa nafasi yao wanamsubiri rais aeleze mafanikio na changamoto zilizopo
badala ya wao kuonesha wanachofanya huko mikoani.
Magazeti yanakeep rekodi kwa muda
mwingi lakini wanataka kuonesha taarifa tu na si makala yanaoonesha
utekelezaji wa malengo ya serikali.
NB
Natumaini wakubwa wakijielemisha na
kutumia wataalamu wao wa habari kujielimisha inaweza kuwa sawa kabisa kwani
kuna mafanikio mengi katika afya, barabara na elimu lakini namna ya kujieleza
ngumu watu wanatukana wanashindwa kutafuta muda wa kueleza mafanikio.
Kwanza elimu watu wameanza kujua
wanahitaji nini kwa sababu elimu imewafikia wengi sasa wanataka ubora. Afya
sasa watu wanatumia hospitali na wanajua wanahitaji nini. Barabara sasa
tunaweza kuhamisha mazao na watu uchumi unabadilika wanataka umeme
wanataka vitu ambavyo ukiwa maskini huwezi kuvipata.
Vyombo vya habari muhimu kuelezea sera,
utekelezaji na pia changamoto zilizopo lakini wanajua kutumia vyema vyombo vya
habari ni wapinzani pekee. Hakika vyombo vya habari vinafanya kazi inayotakiwa
kwa namna unavyoweza kuvitumia na kuwa sumu kama hujui namna ya kuvitumia.
mwisho
COMMENTS