DK. BILAL ACHANGISHA SHS. 105 MILIONI KUHIFADHI MILIMA YA TAO LA MASHARIKI
HomeHabari

DK. BILAL ACHANGISHA SHS. 105 MILIONI KUHIFADHI MILIMA YA TAO LA MASHARIKI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Maalum, Mshauri wa kampuni ya VIP Engineer...

SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MRADI WA GREEN VOICES TANZANIA
WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI ILI KUZALISHA WATAALAM WENYE SIFA
kambi ya wakimbizi yatenga eneo maalumu la albino
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Maalum, Mshauri wa kampuni ya VIP Engineering & Marketing, Fr. James Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha zote na OMR

Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewaomba wadau wa maendeleo na uhifadhi wa mazingira kuisaidia taasisi ya Mfuko wa Udhamini wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) ili kufanikisha uhifadhi wa vyanzo vya maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme nchini.
Dk. Bilal aliyasema hayo jana usiku wakati wa Chakula cha Hisani cha uchangiaji wa mfuko huo wa EAMCEF katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam ambapo alifanikiwa kuchangisha jumla ya Shs. 105.6 milioni.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba wadau wote: taasisi mbalimbali, sekta binafsi, wafanya biashara na washirika wa maendeleo waendelee kuunga mkono uhudi hizi za kuhifadhi misitu ya Milima yaTao la Mashariki kwa kutoa michango ya hali na mali,” alisema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani. Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za EAMCEF ili kuhakikisha kuwa misitu hiyo muhimu kitaifa na kimataifa inaendelea kuchangia ustawi na uboreshaji wa maisha ya jamii na ukuaji wa uchumi wa taifa.Aliwashukuru wadau wote waliochangia katika hafla hiyo na kuwaomba “wadau wengine waige mfano huu mzuri mliouonyesha jioni hii… napenda kuwaomba wale wote walioahidi kutimiza ahadi zao kwani kwa kufanya hivyo mtasaidia kufanikisha mipango iliyokwisha wekwa tayari.”
Katika chakula hicho cha hisani, wadau waliochangia na kiasi cha fedha kikiwa kwenye mabano ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania – TCRA (Shs. 5 milioni), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Shs. 10 milioni), Wakala wa Nishati Vijijini – REA (Shs. 6 milioni), Kampuni ya IPTL-PAP (Shs. 10 milioni), Songas (Shs. 13 milioni), VIP Engineering & Marketing (Shs. 50 milioni) na waratibu wa shughuli hiyo kampuni ya Regalia Media Consult ambayo imechangisha Shs. 1.2 milioni.
Aidha, katika kufanikisha shughuli hiyo, kampuni ya Mabibo Beer, Wines and Spirits ilichangia vinywaji vyenye thamani ya Shs. 2.1 milioni, ITV na Radio One walichangia matangazo yenye thamani ya Shs. 640,000 na Hoteli ya Hyatt Regency walichangia ukumbi na chakula vyote vikiwa na thamani ya Dola 3,000 (takriban Shs. 6.6 milioni).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa Mabibo Beer, Wines & Spirits na Mkurugenzi wa VIP Engineering Marketing Ltd, Benedicta Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPTL, Parthiban Chandrasakaran,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala wa REA, George Nchwale,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, pia kulifanyika mnada wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jamii zinazozunguka misitu hiyo ambazo zimenufaika na miradi ya kijamii inayofadhiliwa na EAMCEF ambapo jumla ya Shs. 4.65 milioni zilikusanywa.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa EAMCEF, Francis Sabuni, alisema kwamba uhifadhi wa Misitu ya Milima ya Tao la Mashariki ni muhimu kijamii, kitaifa na hata kimataifa kwani ndiko kuliko na vyanzo vyote vya maji vinavyotegemewa na mabwawa makubwa matano yanayozalisha umeme nchini Tanzania ambayo ni Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Hale na Pangani.
Sabuni alisema, Milima ya Tao la Mashariki ina eneo la ardhi lenye ukubwa wa takriban kilometa za mraba 5,350 ambalo liko kwenye wilaya 15 ndani ya mikoa mitano.
“Mkoa wa Kilimanjaro kuna Milima ya Upare Kaskazini na Kusini iliyoko katika wilaya za Mwanga na Same; Mkoa wa Tanga kuna Milima ya Usambara Magharibi na Mashariki pamoja na Milima ya Nguu katika wilaya za Lushoto, Korogwe, Muheza, Mkinga na Kilindi na Mkoa wa Dodoma kuna wilaya ya Mpwapwa iliko Milima ya Rubeho,” alisema.
Mikoa mingine ni Morogoro ambako kuna Milima ya Nguru, Uluguru, Ukaguru, Udzungwa, Malundwe, Mahenge na Rubeho ambayo iko katika wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga na Manispaa ya Morogoro, pamoja na Mkoa wa Iringa wenye Milima ya Udzungwa iliyoko kwenye wilaya za Kilolo na Mufindi.
Kwa mujibu wa Sabuni, Milima ya Tao la Mashariki inaunda ukanda wa milima uliopo Mashariki mwa Afrika ambao unatambuliwa duniani kama moja ya maeneo 34 yenye utajiri mkubwa wa bioanuwai na kwa kuwa na viumbe ndwele wengi wanaokabiliwa na tishio la kutoweka.
Bioanuwai ya milimahiyo inatajwa kuwa na manufaa makubwa kijamii katika kupunguza athari za umaskini ambapo mazao ya misitu kama kuni, mbao, madawa ya asili, matunda pori na aina nyingine za vyakula yanakadiriwa kuchangia takriban asilimia 40 ya mahitaji yote ya kaya katika baadhi ya jamii zinazopakana na milima hiyo.
Misitu ya milima hiyo ndiyo vyanzo vikuu pia vya maji ambavyo kwa ujumla hutoa maji kwa matumizi ya viwanda vikubwa nchini pamoja na baadhi ya wananchi wanaokadiriwa kufikia asilimia 25 ya Watanzania wote wanaoishi katika miji ya Iringa, Kilolo, Mufindi, Mpwapwa, Morogoro, Kilosa, Gairo, Mvomero, Mahenge, Ifakara, Muheza, Chalinze, Korogwe, Lushoto, Mwanga, Same, Soni, Mikumi, Kilindi, Handeni, Kibaha pamoja na majiji ya Tanga na Dar es Salaam.
Uzalishaji wa umeme nchini Tanzania unategemea zaidi ustawi wa milima hiyo kwani maji yanayopatikana huko ndiyo hutumika kuzalisha asilimia 90 ya nishati hiyo inayotumia nguvu za maji, ambapo inakadiriwa kwamba asilimia 50 ya umeme wote unaotumika nchini Tanzania huzalishwa katika mabwawa hayo matano yaliyotajwa.
Sabuni anasema, kwa sababu ya kuwa na ardhi yenye rutuba pamoja na mvua za kutosha, milima hiyo ni maarufu kwa kilimo kikubwa cha mpunga, miwa, chai, na kahawa na hivyo kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kufikiwa kwa malengo ya mikakati ya Serikali ya Kilimo Kwanza, SAGCOT na Matokeo Makubwa Sasa (BRN), huku pia ikiwa kivutio kikubwa cha utalii kutokana na kuwa na viumbe ndwele wengi.
“Mto Ruvu ndicho chanzo kikubwa cha maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine, lakini chanzo chake ni Milima ya Uluguru mkoani Morogoro, hivyo bila kuilinda Dar es Salaam itakosa maji na hivyo kuikosesha Tanzania asilimia zaidi ya 70 ya pato lake la taifa kwani maji ya mto huo mbali ya kutumiwa na wanajamii kwa shughuli mbalimbali, lakini pia hutumika viwandani kwa uzalishaji mkubwa wa bidhaa,” anasema Sabuni.
Hata hivyo, inaelezwa kwamba, katika kipindi cha miaka 200 iliyopita, asilimia 70 ya misitu ya Milima ya Tao la Mashariki ilitoweka na kama hali hiyo haitadhibitiwa, kiasi cha misitu kilichobaki kinaweza kutoweka kabisa katika miaka 20 ijayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwakilishi wa ITV na Radio One, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 

Katika kukabiliana na tishio hilo, EAMCEF inashirikisha jamii zinazoizunguka misitu hiyo katika uhifadhi ambapo hutenga asilimia 50 ya rasilimali zake za ufadhili kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kijamii.
“Mfuko unafadhili miradi mbalimbali kwenye Halmashauri za Wilaya 11 ikilenga misitu 9 ya Hifadhi za Mazingira Asilia za Chome na Magamba (Same, Lushoto, Korogwe); Hifadhi za Mazingira Asili za Amani na Nilo (Korogwe, Muheza, Mkinga); Hifadhi za Mazingira Asili za Uluguru na Mkingu (Morogoro Manispaa, Morogoro na Mvomero); Hifadhi za Mazingira Asili za Udzungwa Scaep (Kilombero) na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa (Mufindi, Kilolo na Kilombero),” anafafanua Sabuni.
Sabuni alieleza kwamba, tangu kuanzishwa kwake, EAMCEF imefadhili zaidi ya miradi 200 yenye thamani ya zaidi ya Shs.3.4bilioni ambapo miti zaidi ya milioni 18 imepandwa katika hekta zaidi ya 10,000 kwenye maeneo mbalimbali ya milima hiyo.
“Miradi hiyo katika vijiji zaidi ya 130 ni pamoja na ufugaji wa mbuzi wa maziwa zaidi ya 250, ng’ombe wa maziwa zaidi ya 30, kuku zaidi ya 1,000, nguruwe zaidi ya 100, ufugaji nyuki zaidi ya mizinga ya kisasa 800, majiko banifu zaidi ya 5,000, uwekaji na uimarishaji wa mipaka ya misitu ya hifadhi zaidi ya kilometa 2,000 na kadhalika,” anasema Sabuni.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya EAMCEF, Profesa Gerald Monela, aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kubuni na kuanzisha mfuko huo, kwani kulinda bioanwai zilizoko kwenye misitu ya milioma hiyo ni muhimu zaidi.
“Bioanwai zinazopatika kwenye misitu hii ni adimu na hazipatikani sehemu nyingine duniani, lakini misitu hii ni muhimu kwa upatikanaji wa maji, hivyo ni muhimu sana kuitunza na kuilinda,” alisema.
Profesa Monela aliwashukuru wadau wote waliochangia na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kuunga mkono uhifadhi wa misitu hiyo muhimu kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.


Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,313,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,246,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,Habari,5012,habari dodoma,20,habari. dodoma,31,habaria,1,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,513,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,352,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,2,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: DK. BILAL ACHANGISHA SHS. 105 MILIONI KUHIFADHI MILIMA YA TAO LA MASHARIKI
DK. BILAL ACHANGISHA SHS. 105 MILIONI KUHIFADHI MILIMA YA TAO LA MASHARIKI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjsSEdjFF_vssH2-d5NcxRoQOd2KcB3J_9w-6K8X3X5_MilKbDzQbsoGi_sg1Gn447n-EeDHVcEAGM88yRz915t1dEIaStsKwvEGldISuvAoIvwrqPYmrXmkv33DTCZ8kgkzZZimKA7050Y/s640/14+%25282%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjsSEdjFF_vssH2-d5NcxRoQOd2KcB3J_9w-6K8X3X5_MilKbDzQbsoGi_sg1Gn447n-EeDHVcEAGM88yRz915t1dEIaStsKwvEGldISuvAoIvwrqPYmrXmkv33DTCZ8kgkzZZimKA7050Y/s72-c/14+%25282%2529.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2015/09/dk-bilal-achangisha-shs-105-milioni.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/09/dk-bilal-achangisha-shs-105-milioni.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy